Baada ya miaka ya mapambano na uraibu wa dawa za kulevya, Talik Azizi Mkawa wa Arusha ameamua kufungua ukurasa mpya wa maisha. Akiguswa na wito wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vijana waliokuwa waraibu kujikita kwenye shughuli halali za uzalishaji, Talik ameanza safari ya mabadiliko iliyomrejeshea heshima, afya na matumaini.

Leo, akiwa na kundi la vijana wenzake, Talik anaendesha shamba la mazao ya chakula na biashara linalozalisha maharage, migomba, mihogo, mboga mboga na mpunga.

Anasema kazi imekuwa tiba na dira ya maisha yake, akiwahamasisha vijana wengine kutambua kuwa mabadiliko yanaanza pale mtu anapoamua kuchukua hatua na kuishi maisha yenye malengo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *