
Mvutano unaongezeka tena huko Kinshasa kati ya serikali na kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila. Wakati PPRD imeendelea na shughuli zake za kisiasa, Mahakama Kuu ya Kinshasa/Gombe ilitoa amri mnamo Oktoba 27 kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Jacquemain Shabani, iliyoandikwa Oktoba 18, ya kusimamisha shughuli za chama hicho.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo, PPRD inakataa uamuzi huu na inasisitiza kwamba itaendelea na shughuli zake. Hiki ni kipindi kipya katika mvutano kati ya serikali na chama cha rais wa zamani Joseph Kabila.
Yote yalianza mwezi Aprili mwaka huu. Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza kusimamishwa kiutawala kwa chama cha PPRD, kufuatia uwepo wa Joseph Kabila huko Goma, mji ambao wakati huo ulikuwa chini ya udhibiti wa waasi wa AFC/M23. Lakini siku kumi na nane baadaye, chama cha rais wa zamani kilianza tena shughuli zake, kikisema kwamba sheria ya Kongo inatoa ruhusa ya kuanza tena moja kwa moja shughuli siku kumi na tano baadaye ikiwa hakuna taarifa rasmi iliyopokelewa.
Na kisha, siku ya Jumatatu, Oktoba 27, kipindi kipya kilishuhudiwa: notisi iliyochapishwa katika Mahakama Kuu ya Kinshasa/Gombe ilithibitisha umuhimu wa amri ya kusimamishwa.
PPRD yalaani “uchokozi”
Chama cha PPRD, kwa upande wake, kinasema hakijaona hati hii na kinailaani na kusema kuwa utartibu huo unaendeshwa kisiasa. Emmanuel Ramazani Shadary, katibu wa kudumu wa chama hicho, anazungumza wazi, akitangaza kwamba “ikiwa kusimamishwa huku kupo, hakuhusishi PPRD.” Anazungumzia udikteta, uchokozi usiyokoma kwa chama chake. “Shughuli zinaendelea, mengine ni uchochezi,” anaongeza.
Mvutano huu unakuja wakati Joseph Kabila, aliyehukumiwa kifo na yuko uhamishoni, akijaribu kuchukua tena nafasi ya umma na vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na Kinshasa. Siku tatu zilizopita, jukwaa lake la “Okoa DRC“, lililozinduliwa Nairobi wiki mbili zilizopita, lilifanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari katika mji mkuu.
Bado haijabainika jinsi serikali itakavyoitikia, kwani imekuwa ikiwalenga washirika wa Joseph Kabila kwa miezi kadhaa.