#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Dkt. Mwajuma Hamza, amewataka wasichana wanaotafuta ajira nchini kutojiridhisha na vyeti vya kitaaluma pekee, bali wawe na mtazamo wa kidunia, nidhamu, ujuzi, weledi, ubora na moyo wa kujifunza kila siku bila kuchoka.
Akizungumza mjini Morogoro wakati wa uzinduzi wa umoja wa wanataaluma waliowezeshwa na Shirika la CAMFED ujulikanao kama CAMA Professional, Dkt. Mwajuma amesema wasichana wengi wamekuwa wakitegemea taaluma pekee bila kujali vigezo vya kimaadili na tabia vinavyohitajika katika soko la ajira.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania