#HABARI: Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime, ametahadharisha juu ya uwepo wa kikundi cha watu ambao wanaandaa picha mjongeo na matukio ya nyuma, ambayo yameshashughulikiwa na mengine ni ya kutunga ili wayasambaze yaonekane ndani ya muda mfupi.

DCP Misime amesema wananchi watakapoona picha za aina hiyo kwenye mitandano ya kijamii wasiziamini ni za uongo.

Misime ameongeza kusema kuelekea siku ya uchaguzi usalama upo wa kutosha, hakuna tishio la kiusalama kama ambavyo Jeshi la Polisi liliwahakikishia wananchi Oktoba 26, 2025.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *