#HABARI: Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani Tanzania, imewaasa wanawake na vijana kuwa makini katika kulinda amani, huku ikiwataka kuwa mabalozi wa amani ili kusaidia kujenga kizazi chenye utu na heshima katika jamii.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani, Dkt. Judith Mhina Spendi, katika kongamano la amani la Kitaifa lililoandaliwa na taasisi hiyo lenye lengo la kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu amani na umuhimu wake katika jamii.
Amesema kuwa Tanzania imejijengea sifa ya kuwa nchi ya amani, utulivu na mshikamano kupitia juhudi mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Serikali ikishirikiana na wadau nchini katika kuimarisha hali ya amani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
š±Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 š±kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.