Jamii imeaswa kutosita kutoa au kufichua taarifa za kihalifu kwa mamlaka mbalimbali nchini, kwani ipo Sheria ya Watoa Taarifa na Mashahidi Sura ya 446 ambayo imeundwa mahsusi kuwalinda watoa taarifa na hata kuwalipa fidia chini ya mwongozo wa kanuni za sheria hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Sehemu ya Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Akisa Mhando katika mafunzo maalum kwa waandishi wa habari waliotambuliwa kama wadau muhimu katika utekelezaji wa sheria hiyo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *