Kesho, Watanzania waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kumchagua rais, wabunge, madiwani na wawakilishi.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema maandalizi yote yamekamilika, na vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Matokeo ya uchaguzi wa urais yanatarajiwa kutangazwa ndani ya saa 72 baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi