
Mwandishi wa Saudi Arabia na mchambuzi wa masuala ya kisiasa amejibu matamshi ya dharau yaliyotolewa na Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich akisema, “Ngamia wetu wana asili, lakini nyingi hamna asili.”
Ali Al-Khushaiban, mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Saudi Arabia, amejibu kauli za hivi karibuni za Bezalel Smotrich, Waziri wa Fedha wa Israel, ambaye alisema, ” ikiwa Saudi Arabia itasema inataka kuanzishwa kwa dola la Palestina mkabala wa makubaliano ya kuanzisha uhusiano na Israel, “tutawaambia: Hapana asanteni, marafiki. Endeleeni kupanda ngamia katika jangwa la Saudia.”
Mwandishi huyo ameandika makala katika gazeti la Al-Riyadh akisema: “Israel, ambayo ililazimishwa kumiliki ardhi ya kigeni miongo minane iliyopita, hivi leo inajaribu kujitambulisha kama mmiliki wa historia na ardhi, wakati ngamia wa eneo hili wamekuwa hapa mamilioni ya miaka kabla yao.”
Ali Al-Khushaiban, sambamba na kuashiria kwamba “dharau kwa historia inakuja tu kwa wale ambao hawana historia,” amesema: “Utawala wa Israel (utawala) uliwekwa kwenye eneo (Asia Magharibi) kwa uungaji mkono wa madola yenye nguvu duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na bado inajaribu kuendeleza wazo lisiloweza kutekelezeka kwa kuwaondoa watu wa Palestina.”
Al-Khushaiban amesisitiza kuwa “Saudi Arabia kamwe haitakubali kufutwa taifa la Palestina,” na kuongeza: “Ujumbe wetu wa kisiasa kwa Smotrich na mfano wake ni kwamba haiwezekani kuanzisha uuhuusiano wa kawaida bila dola la Palestina.”
Katika sehemu nyingine ya makala hiyo, mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Saudi Arabia amemhutubu Smotrich kwa kejeli: “Tulijenga nchi yenye ukubwa wa bara kwa ngamia, bila kubomoa nyumba yoyote au kuua binadamu asiye na hatia, hii ni katika hali ambayo nyinyi mnaishi kwenye ardhi isiyo yenu na hata hamjui thamani yake.”