Kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa mpaka kati ya Iran na Afghanistan kimefanyika kwa kuhudhuriwa ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.

Kazem Gharibabadi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Sheria na Masuala ya Kimataifa na Noorullah Noori, Waziri wa Mipaka, Kaumu na Makabila wa Afghanistan walifanya kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa mpaka wa nchi hizo mbili mjini Kabul. Katika mkutano huo ambao ulifanyika katika mazingira ya kujenga na ya kirafiki, mipaka ya Iran na Afghanistan ilitangazwa kuwa mipaka ya urafiki na udugu.

Pande hizo mbili, huku zikielezea utayari wao wa kuimarisha ushirikiano wa mipaka, zilikubaliana kufanya mikutano ya mara kwa mara kati ya wajumbe wa ngazi za juu wa nchi hizo mbili ili kushughulikia masuala ya mipaka. Gharibabadi na Nouri pia walikubaliana kuwa mradi wa kukarabati alama za mpaka unapaswa kuanzishwa tena baada ya kusimama kwa miaka saba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *