Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameahidi kuwa msaidizi mwaminifu na mchapakazi kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan endapo watapewa ridhaa ya kuunda serikali.

Akizungumza Oktoba 28, 2025, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa kufunga kampeni za CCM kitaifa, Dkt. Nchimbi amesema amezunguka katika mikoa 27 ya Tanzania na kujionea kuridhika kwa wananchi kutokana na utekelezaji wa Ilani ya chama hicho chini ya uongozi wa Dkt. Samia.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *