#MICHEZO: Mwanariadha wa Kimataifa wa Mbio Ndefu na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Riadha ya Tanzania, Alphonce Simbu, ameendelea kung’ara Kimataifa baada ya kutajwa kuwania Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mbio za Nje ya Wwanja wa Mwaka, inayotolewa na Shirikisho la Riadha Duniani (World Athletics). Hii ni heshima kubwa kwake na kwa Taifa kwa ujumla, ikionesha jinsi Tanzania inavyozidi kujipatia umaarufu katika tasnia ya michezo, hususan katika riadha.
Akizungumza na ITV Digital, Simbu ambaye hivi karibuni alipeperusha vyema Bendera ya Tanzania kwa kushinda Medali ya Dhahabu, katika Mashindano ya Riadha ya Dunia, amewaomba Watanzania wote pamoja na wadau wa michezo kumpigia kura ili kushinda tuzo hiyo.
Amesema kuwa wapiga kura wanaweza kuingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Shirikisho la Riadha Duniani, kisha kutafuta picha yake na Ku-“like”, hatua itakayohesabika kama kura huku akisisitiza kuwa ushindi wake utakuwa ni fahari ya nchi na motisha kwa wanariadha chipukizi nchini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.