Mshauri mkuu wa kijeshi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametaja “vita vya korido” vinavyoibuka kuwa ni uwanja muhimu katika uhusiano wa kimataifa, na uwanja mpya wa ushawishi wa kimkakati wa Iran.

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa sita wa Kamati ya Kkisayansi ya Mkutano wa “Basij, Maendeleo, na Usalama Endelevu Kusini-mashariki mwa Iran” amesisitiza umuhimu unaoongezeka wa nafasi ya kijeopoliti ya Iran.

“Dunia ya leo inashiriki katika aina mpya ya ushindani unaojulikana kama vita vya korido; ushindani unaofafanuliwa na reli, njia za baharini na barabara za usafirishaji,” amesema Safavi, kamanda mkuu wa zamani wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Ameeleza kuwa katika uwanja huu, “mataifa yenye nafasi ya kimkakati ya kijiografia na usalama imara wa umma yatakuwa wachezaji wakuu.”

Ameongeza kuwa vita vya korido “vinaonyesha ushindani wa staarabu kati ya Mashariki na Magharibi, na kwamba Iran, ikiwa na nafasi yake ya kipekee inayounganisha Mashariki na Magharibi na Kaskazini na Kusini, inaweza kutumika kama mhimili mpya wa mlingano wa [nguvu] wa kikanda.”

Eneo maalumu la kijiografia la Iran, lililoko kando ya korido za kimataifa za Kaskazini-Kusini na Mashariki-Magharibi, ambazo zinaunganisha Asia Magharibi na Asia Mashariki na Ulaya, limeipa nchi hii nafasi ya kipekee ya usafirishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *