Shughuli ya upigaji kura ya mapema Zanzibar imefanyika leo huku malalamiko kadhaa yakiibuka, likiwemo la mgombea uwakilishi wa chama cha ACT-Wazalendo, Omar Saidi Shaabani, aliyedai kuwa mchakato huo ulikuwa na dosari.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, kura ya mapema inawahusu watendaji wa tume, wasimamizi wa uchaguzi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama, kutokana na makundi hayo kuwa na majukumu maalum siku ya uchaguzi mkuu ya kuhakikisha mchakato wa kupiga kura unafanyika kwa amani na usalama.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *