Marekani. Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Sean “Diddy” Combs, anatarajiwa kutoka gerezani Mei 8,2028, katika kifungo chake cha miaka minne na miezi miwili.
Diddy, ambaye alikamatwa Septemba 2024, Oktoba 3,2025 alihukumiwa na mahakama ya New York kwa makosa mawili ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ukahaba. Huku mashtaka makubwa ya sex trafficking na racketeering yakitupiliwa mbali.
Jaji Arun Subramanian alitoa hukumu hiyo, sambamba na faini ya dola 500,000 na masharti ya kifungo cha nje kwa miaka mitano baada ya kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ‘Federal Bureau of Prisons’, Diddy amekuwa akitumikia kifungo chake katika gereza la Metropolitan Detention Center jijini Brooklyn. Tangu kukamatwa kwake huku akitarajiwa kuachiwa Mei 2028 kutokana na kupunguziwa muda wa kukaa gerezani inayojulikana kama ‘Good Conduct Time’.
Hata hivyo, vyanzo vya karibu na gereza hilo vimeeleza kuwa Diddy anaweza kuachiliwa mapema zaidi endapo atajiunga na ‘Residential Drug Abuse Program (RDAP)’, shirika linalosaidia kupunguza muda wa kifungo kwa mtuhumiwa ambapo shirika hilo linaweza kumpunguza kifungo kwa muhusika hadi miezi 12.