
Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ethiopia ugenini huko Addis Ababa, Ethiopia.
Matokeo hayo yameifanya Twiga Stars ijihakikishie kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0 ikibebwa na ushindi wa mabao 2-0 ilioupata katika mechi ya kwanza hapa Dar es Salaam.
Bao pekee lililoihakikishia Twiga Stars ushindi katika mechi ya leo linefungwa na Diana Lucas.
Kufuzu huko kutaifanya Twiga Stars ishiriki Fainali za WAFCON kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo mwaka 2010 na mwaka 2024.
Fainali za WAFCON 2026 ndizozitatumika kusaka timu nneambazo zitaiwakilisha Afrikakatika Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitafanyika Brazil 2027.
Timu hizo ni ambazo zitamaliza katika nafasi nne za juu katika Fainali za WAFCON 2026 ambazo
zimepangwa kufanyika kuanzia Machi 17 hadi Aprili Aprili 3, mwakani.