Wamiliki wa shule nchini wamehimizwa kuwekeza mapema katika mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili kujenga kizazi chenye uelewa wa teknolojia tangu utotoni.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Biashara ya Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Julius Kessy, wakati wa kukabidhi kompyuta 15 zenye thamani ya shilingi milioni 32 kwa Shule ya Msingi Canossa, jijini Dar es Salaam.
Kessy amesema uwekezaji wa mapema kwenye TEHAMA unawaandaa wanafunzi kwa dunia ya kisasa inayotegemea teknolojia.
Akipokea vifaa hivyo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sister Demetria Komugasho, amesema msaada huo utasaidia kuwajengea watoto msingi wa udadisi na uelewa wa kidijitali.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates