
Operesheni ya nguvu inaofanywa na vikosi vya usalama hufanyika mara kwa mara huko Rio de Janeiro, licha ya ufanisi wake unaopingwa. Lakini siku ya Jumanne, mitaa ya Rio de Janeiro ilikumbwa na hali nzito. Angalau watu 64 waliuawa katika operesheni kali zaidi ya polisi katika historia ya jiji hilo, iliyozinduliwa dhidi ya moja ya magenge yanayojihusosha na biashara ya dawa za kulevya nchini Brazili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Operesheni hizi hulenga kwa ujumla vitongoji maskini na vyenye watu wengi ambavyo mara nyingi huishi chini ya udhibiti wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Lakini operesheni ya Jumanne, kutokana na ukubwa na vurugu zake, ilisababisha mshtuko mkubwa. Hata Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa imeelezea hofu yake na kutoa wito wa uchunguzi wa haraka. Gavana wa mrengo wa kulia wa jimbo la Rio, Claudio Castro, ametangaza kwamba wahalifu 60 waliangamizwa. Maafisa wanne wa polisi pia waliuawa, chanzo ndani ya idara yake kimesema.
Operesheni hiyo, iliyojumuisha maafisa 2,500, ililenga katika majengo mawili ya maeneo ya watu masikini kaskazini mwa Rio, Complexo da Penha na Complexo do Alemão, yaliyoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa. Katika Hospitali ya Getulio Vargas, ambapo milipuko ya risasi iliweza kusikika karibu, magari magari yakibeba maiti na majeruhi wa risasi iliiendelea kuoneka katika hospitali za mji huo.