Kimbunga chenye nguvu cha Melissa kinaelekea Cuba baada ya kuiathiri vibaya Jamaika leo Jumatano, Oktoba 28. Mamlaka imeitangaza Jamaica kuwa “eneo la maafa.” Miundombinu kadhaa imeharibiwa na maeneo mengi amekumbwa na mafuriko. Kwa upepo unaoendelea kukaribia kilomita 300 kwa saa, kimbunga hicho, kilichowekwa katika Kategoria ya 5—ya juu zaidi katika kipimo cha Saffir-Simpson—kimetua magharibi mwa Jamaica saa sita mchana, saa za Jamaika.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hiki ndicho kimbunga kibaya zaidi kuikumba Jamaika tangu mwanzo wa rekodi za hali ya hewa. Waziri Mkuu Andrew Holmes amekitangaza kisiwa hicho kuwa “eneo la maafa” siku ya Jumanne Oktoba 28. Picha za kwanza zilizotolewa na vyombo vya habari vya ndani zinaonyesha uharibifu mkubwa. Wajamaica walipigwa na upepo mkali sana, mvua kubwa, na mawimbi yenye urefu wa mita kadhaa.

Mkoa ulioathiriwa zaidi unaonekana kuwa ambapo kimbunga hicho kilitua, amesema Desmond McKensey, Waziri wa Serikali katika eneo hilo, katika mkutano na waandishi wa habari. Saint Elizabeth, parokia iliyo kusini magharibi mwa kisiwa chenye wakaazi 150,000 na kinachochukuliwa kuwa “hifadhi kuu ya ngano” ya Jamaika, kimekumbwa na mafuriko makubwa. “Parokia ya Saint Elizabeth iko chini ya maji kabisa. Uharibifu ni mkubwa… Jamaika yote imeathiriwa na kimbunga Melissa. Barabara zimekatwa kote nchini. Karibu kila parokia imeathiriwa na barabara zilizofungwa, miti iliyong’olewa, na miundombinu iliyoharibiwa. Na mafuriko yanaathiri jamii nyingi,” ameongeza, akibainisha kuwa hospitali kadhaa zimeharibiwa.

Baada ya kudhoofika kidogo na kushushwa hadi Kategoria ya 4, kimbunga Melissa kilianza kuhama kutoka Jamaika kuelekea Cuba karibu saa 9:00 usiku, kulingana na Kituo cha taifa cha Vimbunga cha Marekani (NHC).”

Huko Cuba, wakazi wanakimbia pwani kimbunga Melissa kinapokaribia. Mamlaka imetangaza hali ya tahadhari katika majimbo sita ya mashariki, na wakazi wamekuwa wakihifadhi chakula, mishumaa, na betri tangu siku ya  Jumatatu.

Siku ya Jumanne Umoja wa Mataifa ulitangaza nia yake ya kusafirisha kwa ndege vifaa vya misaada takriban 2,000 hadi Jamaica kutoka Barbados haraka iwezekanavyo. Kimbunga kikubwa cha mwisho kuikumba Jamaika kilikuwa Gilbert, mnamo mwezi Septemba 1988. Kimbunga hicho kiliua watu 40 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Nchi hiyo, ambayo uchumi wake unategemea sana utalii, ilikuwa imefunga uwanja wake wa ndege wa kimataifa na bandari za juu. Ingawa baadhi ya watalii waliweza kuondoka nchini, wengine 25,000 walibaki, serikali imeripoti. Kama wakazi, waliagizwa kujificha katika vyumba vya hoteli, na kusubiri hadi kimbunga kimalize kupita kabla ya kutoka nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *