Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameshiriki zoezi la kupiga kura kumchagua diwani, mbunge na Rais wa Tanzania kwenye Kituo kilichopo Shule ya Sekondari Kwaraa, Babati mjini.
Mara baada ya kupiga kura, Sendiga ametoa rai kwa wananchi walioko nyumbani kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vyao vya kupigia kura, akiendelea kusisitiza amani na usalama wa kutosha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo sambamba na kutokuwepo kwa msongamano wa watu kwenye vituo hivyo.
✍ Hellen Kawiche
#AzamTVUpdates #UchaguziMkuu2025