
Mazungumzo kati ya Afghanistan na Pakistan kwa ajili ya usitishaji mapigano wa kudumu kufuatia mapigano yao ya hivi karibuni yaliyosababisha vifo vingi, yameshindwa, Islamabad ilmetangaza leo Jumatano, Oktoba 29, huku mazungumzo yakikwama.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Kwa bahati mbaya, upande wa Afghanistan haukutoa hakikisho lolote, imendelea kupuuza suala kuu, na kutumia mchezo wa lawama, ukwepaji, na ujanja,” Waziri wa Habari wa Pakistan ametangaza kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Baada ya majadiliano ya siku nne huko Istanbul, yaliyosimamiwa na Qatar na Uturuki, “kwa hivyo mazungumzo hayajafanikiwa kutoa suluhisho lolote linalowezekana,” amelalamika.
Makabiliano hayo, ya kiwango kisicho cha kawaida, yalianza wiki mbili zilizopita wakati serikali ya Taliban ilipoanzisha shambulio kwenye mpaka baada ya milipuko huko Kabul ambayo yalihusishwa Pakistan.