Rais Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kushinda muhula wa pili katika uchaguzi unaofanyika leo, hasa baada ya wapinzani wake wakuu ama kususia uchaguzi au kuenguliwa. Zoezi la upigaji kura limeanza bila msisimko mkubwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Licha ya CCM kuonekana kutokuwa na mpinzani wa moja kwa moja, chama hicho kinakabiliwa na upinzani wa kimtazamo kutoka kwa raia, wanaharakati, viongozi wa dini na baadhi ya makundi ya kimataifa yanayokosoa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa madai ya kukandamiza haki za binadamu na uhuru wa kisiasa. 

Polisi wamekabiliana na ‘waandamanaji’ jijini Dar es Salaam wakati kura zikiendelea kupigwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Polisi jijini Dar es Salaam wametawanya kundi la vijana waliokuwa wakijaribu kuandamana katika eneo la Ubongo na Kimara eneo la Kibo, wakati huu wa uchaguzi mkuu unaoendelea nchini.

Alfred Chalamila: Ole wao watakaojaribu kuvuruga uchaguzi 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Chalamila, amesema vyombo vya dola viko imara na tayari kukabiliana na jaribio lolote la uvunjifu wa amani katika jiji hilo, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuvuruga utulivu.

Watu kuhamasiswa kupiga kura

Idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza katika jiji kuu la Tanzania, Dar es Salaam, leo kwa zoezi la uchaguzi huku wapinzani wakuu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa aidha wamefungwa jela ama kuzuiwa kugombea.

Afisa mmoja kutoka chama tawala, Chama cha Mapinduzi, CCM wilayani Temeke  Dar es Salaam, aliyezungumza na shirika la habari la Agence France Press (AFP) kwa sharti la kutotajwa jina, amesema watawahamasisha watu mitaani na majumbani kutoka na kupiga kura.

Awali shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilaani kile ilichokitaja kuwa “wimbi la ugaidi” kabla ya uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na “kutoweka na kuteswa kwa watu pamoja na mauaji ya kiholela ya viongozi wa upinzani na wanaharakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *