Kongamano kuhusu amani katika eneo la Maziwa Makuu, linafanyika Alhamisi hii jijini Paris nchini Ufaransa, ambapo wadau mbalimbali wanatarajiwa kutoa mchango wa kifedha kupambana na hali mbaya ya kibinadamu hasa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mzozo wa Mashariki mwa DRC, umesambaa hadi katika nchi jirani za Burundi, Rwanda na Uganda ambazo zimeendelea kuwapokea maelfu ya wakimbizi.

Wakati kongamano hilo likifanyika nchini DRC pekee, kuna wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni saba, wakiwemo wengine 500,000 ambao wamekimbilia Uganda na wengine Rwanda na Burundi.

Rais Felix Tshisekedi ni miongoni mwa viongozi kutoka eneo la Maziwa Makuu anayehudhuria kongamano hilo, lakini viongozi wa nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda, ripoti zinasema hawatokuwepo.

Msuluhishi wa mzozo wa DRC kutoka Umoja wa Afrika, rais wa Togo Faure Gnassingbé, na mwakilishi wa Qatar ambayo pia ni mpatanishi wa mzozo unaoendelea atahuhduiria pia.

Mbali na kutafuta msaada wa fedha, watakaohudhuria kongaman hilo wanatarajiwa kusisitiza uungwaji mkono wa mikataba ya Doha na Washington, kusaidia kuleta amani ya kudumu kwenye ukanda huo wa Maziwa Makuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *