Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Aidarous, amewahakikishia wananchi wa visiwa hivyo kwamba matokeo rasmi ya uchaguzi yatatangazwa rasmi leo Alhamisi jioni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shughuli ya kuhesabu kura huko visiwani Zanzibar ilianza baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa saa kumi jioni jana Jumatano Oktoba 29.

Kwa upande mwingine shughuli ya upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa Tanzania imekamilika licha ya maandamano ya wafuasi wa upinzani kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo kushudiwa katika miji tofauti ya Tanzania bara.

Baadab ya kutokea kwa maandamano yenye ghasia katika jiji kuu la kibiashara nchini Tanzania, polisi nchini humo ilitangaza amri ya kutotoka nje baada ya saa kumi na mbili jioni, lakini hata baada ya muda huo kupitia mitandao ya kijamii maandamano bado yalikuwa yanaendelea.

Waandamanaji wanadai kuchukizwa na kubinywa kwa demokrasia, haki na kuchoshwa na madai ya kutekwa nyara kwa wakosoaji wa serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Hata hivyo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushinda kufuatia kuenguliwa kwa wagombea wakuu wa upinzani.

Hapo jana siku ya uchaguzi, shirika la kimataifa la uchunguzi wa mtandao wa Netblocks, lilisema kuwa limegundua kubinywa kwa mtandao kote nchini humo.

Serikali yawaagiza wafanyakazi wa umma kufanyia kazi nyumbani

Serikali ya Tanzania imewataka watumishi wa umma kufanyia kazi nyumbani leo, Oktoba 30, 2025. Msemaji wa serikali, Gerson Msigwa, aliweka ujumbe kwenye mtandao wake wa Instagram akielezea tangazo hilo kuwa kufuatia angalizo la kiusalama lililotolewa na jeshi la polisi kwa wakaazi wa jiji la Dar es Salaam watafanyia kazi nyumbani.

“Kesho tarehe 30 Oktoba 2025, watumishi wote wa umma nchini wafanyiekazi nyumbani isipokuwa wale ambao majukumu yao ya kazi yanawakata kuwepo katika vituo vyao vya kazi kama ambavyo wataelekezwa na waajiri wao.”

Taarifa hiyo pia ilionyesha kuwa waajiri wa sekta binafsi wanashauriwa kuzingatia tahadhari hiyo.

Marekani yawashauri wafanyakazi wake kuchukuwa tahadhari

Marekani kupitia ubalozi wake nchini Tanzania, umeataka wafanyakazi wa Serikali wanaoishi nchini Tanzania  kuchukuwa tahadhari na kujilinda kufuatia ghasia na maandamano yalioripotiwa nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *