Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa, nchi yake inawasiliana na pande zote mbili, Palestina na Israel, ili kudumisha usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, amesema kuwa nchi yake inawasiliana kwa dhati na pande zote mbili za Israel na Palestina ili kuhakikisha kunatekelezwa makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza, licha ya changamoto ilizokumbana nazo.

Aliongeza: “Tunafuatilia changamoto ambazo usitishaji vita ulikumbana nazo Jumanne ya wiki hii, na hilo lilitarajiwa. Hata hivyo, kwa bahati nzuri, pande zote mbili zinakubali kwamba makubaliano haya lazima yatekelezwe kikamilifu.”

Israel, ambayo imekuwa ikishambulia Ukanda wa Gaza mara kwa mara kinyume na makubaliano ya kusitisha mapigano, iliilaumu Hamas kuwa imekiuka makubaliano hayo, ikidai kundi hilo lilishambulia wanajeshi wa utawala huko huko Rafah siku ya Jumanne, na kwamba mwanajeshi mmoja aliuawa.

Wakati huuo huo, mashambulizi yaliyofanywa siku ya Jumatano na utawala ghasibu wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza yaliua Wapalestina wasiopungua 100, wakiwemo watoto 35, ukiwa ni ukiukaji wa hivi karibuni wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na utawala huo ghasibu.

Katika upande mwingine Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeonya kwamba uharibifu unaoendelea ambao umesababishwa na vita vya Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya elimu, umeweka mustakabali wa mamilioni ya watoto wa Kipalestina hatarini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *