Israel imetambua mabaki ya mateka Amiram Kuper na Sahar Baruch, ambao miili yao ilikabidhiwa na Hamas mapema leo, taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imetangaza siku ya Alhamisi, Oktoba 30.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo inabainisha kwamba familia za marehemu ziliarifiwa baada ya “kukamilika kwa mchakato wa utambuzi na Taasisi ya kitaifa ya Uchunguzi na Tiba.”

Sahar Baruch alitekwa nyara kutoka Kibbutz Beeri mnamo Oktoba 7, 2023, na kupelekwa Gaza, ambapo aliuawa katika operesheni ya uokoaji ya jeshi iliyoshindwa miezi miwili baadaye. Alikuwa na umri wa miaka 25 wakati wa kifo chake.

Amiram Kuper, mwenye umri wa miaka 84 wakati wa kutekwa nyara kwake, alitekwa nyara pamoja na mkewe, Nourit, kutoka nyumbani kwao Kibbutz Nir Oz.

Israel ilitangaza kifo chake akiwa mikononi mwa watekaji nyara huko Gaza mnamo Juni 2024. Tawi la Hamas lilirudisha miili hiyo miwili kwa shirika la Msalaba Mwekundu siku ya Alhamisi, kisha shirika hilo liliikabidhi kwa jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza, kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutumika tangu Oktoba 10.

Kikosi cha Ezzedine al-Qassam kilitangaza mapema alasiri siku ya Alhamisi kwenye kituo chao ca Telegram kwamba kitakabidhi miili ya mateka wawili waliofariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *