Jeshi nchini Guinea-Bissau limethibitisha kuzima kile linasema ni jaribio la kuvuruga mpangilio wa kikatiba ambapo maofisa wa ngazi ya juu wa jeshi wamekatamatwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais.

Kampeni zinatarajiwa kuanza Jumamosi ya wiki hii nchini Guinea-Bissau, wiki tatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge   na urais, uchaguzi ambao Rais  wa sasa Umaro Sissoco Embalo anatarajiwa kuibuka na ushindi baada ya mpinzani wake mkuu kuzuiliwa kushiriki.

Embalo baada ya kikao cha baraza la Mawaziri siku ya Alhamisi aliwaambia wanahabari kwamba vurugu hazitokubalika akiongeza kuwa serikali yake imechukua kila tahadhari kuhakikisha usalama wa kila mgombea wakati wa kampeni.

Brigadier Jenerali Daba Nawalna, mkuu wa kituo cha kutoa mafunzo ya kijeshi karibia kilomita 30 sawa na maili 18 kutoka Mji mkuu wa nchi ya Bissau, anatuhumiwa kwa kupanga njama hiyo ya mapinduzi na alikuwa miongoni mwa waliokamatwa kwa mujibu wa jeshi.

Guinea-Bissau ina historia ya mapunduzi ya kijeshi tangu uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka wa  1974 ila tangu wakati wa uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2014, hiyo imeonekana kuelekea katika mkondo wa kuheshimu utawala wa kiraia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *