Nchini Afrika Kusini, mahakama zinaandika upya historia. Mahakama imekanusha, Alhamisi, Oktoba 30, maelezo rasmi ya kifo cha mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Albert Luthuli. Hakuuawa kwa kugongwa na treni mnamo mwaka 1967, kama ilivyodaiwa na mamlaka wakati huo, bali na shambulio kutoka kwa vikosi vya usalama vya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès

Ingawa hakuna uwezekano kwamba washukiwa wowote sasa watashtakiwa, ikizingatiwa kwamba wamekufa au hawawezi kupatikana, uamuzi huu ni muhimu kwa nchi nzima.

Jaji katika mahakama ya Pietermaritzburg mashariki mwa Afrika Kusini ameamua: Albert Luthuli aliuawa na maafisa wa kitengo maalum cha polisi wa ubaguzi wa rangi, kama familia yake imekuwa ikisisitiza kila wakati. Mauaji hayo yalifichwa, kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa kampuni ya reli ya Afrika Kusini, ili ionekane kwa alifariki ajali ajali ya barabarani baada ya kugongwa na treni.

Jaji alipuuza matokeo ya uchunguzi wa mwaka 1967 na kuwataja wanaume saba, ambao mahakama haikuweza kuwapata, kama waliofanya mauaji hayo au waliofanya kazi kama washirika. Miongoni mwao ni dereva wa treni, afisa mooja wa idara ya zimamoto, mkuu wa kituo, na maafisa wawili wa polisi wa reli. Uamuzi huu unabatilisha matokeo ya uchunguzi wa mwaka 1967 na kurejesha ukweli, miaka 58 baada ya matukio hayo, kwa kuridhika sana kwa familia ya kiongozi wa zamani wa ANC, chama cha ukombozi cha Afrika Kusini.

Albert Luthuli aliongoza ANC kuanzia mwaka 1952 hadi kifo chake, kipindi ambacho utawala wa ubaguzi wa rangi ulipiga marufuku chama hicho mwaka wa 1960. Katika sherehe ya Tuzo ya Amani ya Nobel huko Oslo mwaka wa 1961, Luthuli alitoa ombi la dhati la kutotumia vurugu.

“Kurekebisha upotoshaji wa zamani wa historia”

Chama chake pia kimekaribisha hitimisho la mahakama ya Pietermaritzburg, katika taarifa inayotambua matokeo ya uchunguzi huu, ambao “unarekebisha upotoshaji wa zamani wa historia” na unawakilisha “ushindi wa kimaadili si tu kwa familia yake, bali pia kwa mashahidi wote wa mapambano yetu ambao maisha yao yalichukuliwa na utawala katili wa ubaguzi wa rangi.” 

Uchunguzi kuhusu sababu za kifo chake ulifunguliwa tena mwezi Aprili 2025, kama sehemu ya mapitio ya watu kutoweka na vurugu za kisiasa zilizofanywa wakati wa ubaguzi wa rangi, ambazo zilimalizika mwanzoni mwa miaka ya 1990. Uchunguzi upya wa kifo hiki cha kutiliwa shaka ni mojawapo ya mifano ya hivi karibuni ya utayari wa upande wa mashtaka wa Afrika Kusini kufungua tena kesi za zamani za uhalifu zilizofanywa na utawala wa ubaguzi wa rangi ambazo hazijaadhibiwa, chini ya shinikizo kutoka kwa familia za waathiriwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *