
Mohammad al-Farah, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amejibu matamshi ya Waziri wa Vita wa Israel kwamba utawala huo ghasibu bado haujafikia malengo yake yoyote hadi sasa.
Katika radiamali yake kwa tishio la Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz, Mohammed al-Farah, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa “hatutamtuhusu mtenda jinai atutishe.”
Jana, katika sherehe za kuhitimu kwa wanachuo wa kijeshi, Waziri wa Vita wa Israel alidai kuhusu Yemen kwamba “Israel bado haijawa na kauli ya mwisho.”
Alisema kuwa, “Wahouthi watalipa gharama kubwa kwa juhudi zao za kulenga eneo la ndani la Israeli katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Bado hatujafikia uamuzi wa mwisho kuhusu hili,” alisema.
Itakumbukwa kuwa, Yemen imefanya imefanya mashambulizi mengi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel tangu kuanza vita Gaza. Mashambulizi hayo yote yalifanywa na Yemen ili kuwaunga mkono Wapalestina na ili kuishinikiza Tel Aviv ikomeshe jinai zake kwenye Ukanda wa Ghaza iliouzingira kila upande.
Mengi ya mashambulio ya Yemen yalilenga maeneo ya kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni hasa eneo la Eilat, lakini baadhi ya droni na makombora yalikuwa yanapiga ndani zaidi ikiwa ni pamoja na Tel Aviv na hasa Uwanja wa Ndege wa Ben-Gurion.
Mashambulizi hayo yalikuwa ni shinikizo kubwa la kiusalama kwa Israel na hata mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Yemen hayakulizuia taifa hilo shujaa kuitia adabu Israel.
