
Serikali ya Rais Donald Trump, imesema itaenda kudhibiti idadi ya wakimbizi watakaoruhusiwa kuingia nchini humo kuanzia mwaka ujao hadi kufikia elfu 7 na 500, na kwamba nafasi hizo zitajazwa kwa sehemu kubwa na wazungu kutoka Afrika Kusini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa sera mpya, idadi kubwa ya watakaokubaliwa itakuwa waafrika na wahusika wengine wasio na haki katika nchi zao.
Rais Donald Trump alisitisha kwa kiasi kikubwa uhamishaji wa wakimbizi baada ya kuingia madarakani lakini ametoa msamaha kwa wananchi wa taifa la Afrika Kusini licha ya serikali ya Pretoria kusisitiza kuwa hawabaguliwi.
Tangu kundi la kwanza la waafrika kutoka Afrika Kusini kuhamia Marekani mwezi Mei, Rais Trump aliendesha kampeni ya kuwafukuza wahamiaji wasio na vibali na kusaini agizo la Marekani kutopokea wakimbizi Zaidi.
