Lengo kuu la mpango huu ni kuimarisha haki za wanawake na wasichana, hususan wale wenye ulemavu, kwa kukabiliana na changamoto kama ukeketaji , ndoa za utotoni, na ukatili wa kijinsia. Bi Desteria Anyanga, Afisa wa Jinsia katika Wizara ya Afya Tanzania, anaeleza kuwa “Kwa msaada wa fedha kutoka katika mradi wa Chaguo Langu, Haki Yangu, tuliweza kupata rasilimali zilizotuwezesha kuridhia na kuimarisha miongozo yetu ya utoaji huduma zenye kuzingatia usawa wa kijinsia.”

Mradi wa "Chaguo Langu Haki Yangu" umewawezesha wanawake na wasichana na kuwasaidia kuondokana na mila potofu ya ukeketaji na ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Mradi wa “Chaguo Langu Haki Yangu” umewawezesha wanawake na wasichana na kuwasaidia kuondokana na mila potofu ya ukeketaji na ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Kwa upande wa Zanzibar, programu imeleta mwamko mkubwa wa kijamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu. Bw. Abushir Saidi Khatib, Afisa Mpango Mwandamizi kutoka Baraza la Taifa la watu wenye Ulemavu (NDC), anasema

Watu wenye ulemavu wamepata mwamko mkubwa, na jamii pia imeanza kuelewa na kuheshimu haki zao. Wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu sasa wanajitokeza kujifunza zaidi kuhusu haki za msingi za watoto wao.”

Idara ya Maendeleo ya Watoto imetaja mafanikio muhimu ya miundombinu iliyojengwa kupitia programu hii. Sebastian F. Kitiku, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto, anabainisha kuwa “Kupitia programu ya Chaguo Langu, Haki Yangu, tumefanikiwa kujenga vituo viwili jumuishi na kuvipatia vifaa kamili katika wilaya za Tarime na Kishapu.”

Wasichana wengi wamepata mafunzo ya stadi za maisha na fursa za kiuchumi.
 

Esther Brighton, mnufaika wa mradi, anasema, “Nimepiga hatua kubwa sana tangu nilipojiunga na mradi huu. Nilipata nafasi ya kusoma VETA, na sasa nina uwezo wa kumhudumia mwanangu bila kutegemea wazazi. Maisha yangu yamebadilika kabisa.”

Mradi wa "Chaguo Langu Haki Yangu" umewawezesha wanawake na wasichana na kuwasaidia kuondokana na mila potofu ya ukeketaji na ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Mradi wa “Chaguo Langu Haki Yangu” umewawezesha wanawake na wasichana na kuwasaidia kuondokana na mila potofu ya ukeketaji na ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Baada ya mafunzo, washiriki hupatiwa vitendea kazi ili kuanzisha biashara ndogo ndogo.

Mariam M. Adam, mmoja wa walionufaika, anasimulia akisema “Baada ya kumaliza mafunzo tulipewa vifaa vya kazi ,ikiwemo vya kupikia na kupambia. Nilianza kutengeneza keki na kufanikiwa kujikimu kimaisha. Nilifurahi sana kuona ahadi zikitimizwa; nilijikuta nalia kwa furaha.”

Mhitimu wa mafunzo katika kituo cha ATFGM Masanga ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya faragha yake  anasema,

Nina furaha kubwa kuwa sehemu ya programu hii. Nimejifunza mengi na sasa nina uwezo wa kusaidia wenzangu kuepuka ukeketaji, ambao unaathiri maisha yetu, elimu na afya.”

Mark Bryan Schreiner, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania, anasisitiza umuhimu wa huduma jumuishi kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia akisema, “Kituo cha Hesperian kitatoa huduma jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, kuhakikisha wanapata matunzo na msaada bila ubaguzi au unyanyapaa. Hii ni hatua muhimu kuelekea usawa wa kweli na hadhi kwa kila mwanamke na msichana.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *