Nchini Sudan Wanamgambo wa RSF Wamesema kwamba wamewakamata wapiganaji kadhaa wanaotuhumiwa kutekeleza vitendo vya uhalifu na unyanyasaji wakati wa kutekwa kwa mji wa El-Fasher.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vikosi hivyo vya RSF viliitoa taarifa hiyo jana jioni, kwamba wapiganaji kadhaa wanaoshutumiwa kufanya unyanyasaji wakati wa kuudhibiti mji wa magharibi wa El-Fasher, wamekamatwa.

Haya yanajiri wakati afisa wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Tom Fletcher, ameliambia Baraza la Usalama kwamba kulikuwa na ripoti za kuaminika za mauaji makubwa baada ya RSF kuingia El-Fasher, na kuonya kwamba utisho unaendelea huko Darfur na Kordofan jirani.

Mji wa El-Fasher nchini Sudan umekuwa kitovu cha makabiliano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF.
Mji wa El-Fasher nchini Sudan umekuwa kitovu cha makabiliano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF. © Airbus DS 2025 via AP

Wakati huo huo Umoja wa mataifa unadai kuwawajibisha wakuu viongozi wa kundi hilo, na kusema kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa mapema basi mauaji ya kikatili yataendelea eneo hilo..Kwa upande wake Kundi hilo la RSF pia limethibitisha kufuata sheria, kanuni za maadili na nidhamu ya kijeshi wakati wa vita.

Wanamgambo wa RSF wanashutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu tangu walipoingia El-Fasher video kadhaa zikionyesha mauaji ya kiholela katika hospitali moja watoto wakipigwa risasi mbele ya wazazi wao, na raia wakipigwa na kuibiwa walipokuwa wakikimbia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *