Karibia watu 700 wameuawa nchini Tanzania katika kipindi cha siku tatu kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi kulingana na taarifa ya chama kikuu cha upinzani Chadema.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye serikali yake inatuhumiwa kwa ukandamizaji wa haki za binadamu na kutumia mkono wa chuma dhidi ya wapinzani, baadhi wakiwa wamezuiwa gerezani wakati wengine wakizuiwa kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Uchaguzi wa Jumatano uligeuka kuwa wa vurugu, waandamanaji wakijitokeza kwenye jijini kuu la Dar es Salaam na Miji mingine, wakiharibu mabango ya Rais Samia pamoja na kuvamia vituo vya kupiga kura hali iliyoplekea kuzimwa kwa intaneti na kutangazwa kwa makataa ya watu kutotembea nje.

Watu wakiandamana jijini Arusha, Tanzania, Siku ya Uchaguzi mkuu Jumatano, Oct. 29, 2025. (AP Photo/str)
Watu wakiandamana jijini Arusha, Tanzania, Siku ya Uchaguzi mkuu Jumatano, Oct. 29, 2025. (AP Photo/str) AP

Wakati wanahabari wa kigeni wakiwa wamezuiwa kufuatilia uchaguzi huo, imekuwa vigumu kupata taarifa ya kinachojiri nchini Tanzania.

Chama kikuu cha upinzani Chadema ambacho kilizuiwa kushirki uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kimethibitisha kuwa waandamanaji wameendelea kuingia katika jiji kuu la Dar es Salaam leo Ijumaa.

“Tunapozungumza, idadi ya watu waliofariki jijini Dar (es Salaam) inakaribia  watu  350 wakati wengine zaidi ya 200 wakiwa wamefariki jijini Mwanza. Tukiongeza idadi ya watu waliofariki kutoka katika maeneo mengine ya nchi, idadi kamili inakaribia 700,”  alisema Msemaji wa Chadema John Kitoka.

Polisi wakiwa katika mitaa ya Zanzibar, Tanzania, Alhamis, Oct. 30, 2025. (AP Photo)
Polisi wakiwa katika mitaa ya Zanzibar, Tanzania, Alhamis, Oct. 30, 2025. (AP Photo) AP

“Idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa,” alionya akisema huenda watu wanauawa wakati wa usiku haswa makataa ya kutembea nje yakiwa yametangazwa.

Chanzo cha kiusalama kimeiambia AFP kuwa walikuwa wanapokea taarifa ya idadi ya watu waliofariki kuwa zaidi ya 500, au 700-800 kote nchini wakati Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty likisema limepokea taarifa kuwa karibia watu 100 wamefariki.

Hosipitali mbalimbali na vituo vya afya havikutaka kuwasiliana na AFP mooja kwa moja kuhusu suala hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *