Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania INEC, Jaji Jacob Mwambegele, matokeo ya awali katika majimbo 19 ambayo kura zake zimekwisha hesabiwa hadi sasa, yanammpa mgombea urais wa Chama cha CCM, Samia Suluhu Hassan ushindi wa zaidi ya asilimia 94 dhidi ya wagombea 16 anaochuana nao. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa Urais wa chama cha mapinduzi CCM nchini Tanzania,Samia Suluhu Hassan, anaongoza kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa kutoka majimbo 19, kulingana na Tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania, INEC.

Wakati huo huo INEC imesema itatangaza mshindi wa nafasi ya urais ndani ya saa 72 baada ya kukamilika zoezi la kupiga kura. 

Kwa upande mwingine Mkuu wa jeshi nchini Tanzania amelaani vitendo vya vurgu vinavyoendelea kote nchini humo na kuvitaja kuwa kinyume cha sheria.

Katika hotuba yake iliyorushwa na televisheni ya taifa, Jenerali Jacob John Mkunda alisema ni ‘lazima utawala wa sheria uzingatiwe’ na kuonya kuwa wahusika watachukuliwa hatua.

Hayo yanajiri wakati wabunge wa umoja wa Ulaya (EU), hapo jana jioni walitoa tamko la Pamoja kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania waliosema haukuwa huru wala wa haki, wakizitaka nchi washirika na wadau wa demokrasia kukemea kilichofanyika.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Ulaya, David McAllister, kile kilichopaswa kuonekana kama kusherehekea demokrasia, kiligeuka kuwa vitisho, hofu na ukandamizwaji wa haki za watu.

McAllister kwenye taarifa yake ameongeza kuwa uchaguzi uliofanyika hapo jana haupaswi kutambuliwa kama uchaguzi huru na haki, kwakuwa udanganyifu haukuanzia kwenye sanduku la kura peke yake bali ulianza miezi kadhaa nyuma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *