Kwa sababu zaidi ya watu bilioni 4.4  zaidi ya nusu ya watu wote duniani  wanaishi mijini, na idadi hii inatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 70 kufikia mwaka 2050, Kwa kutumia mwongozo mpya wa “Kuchukua Mtazamo wa Kimkakati kwa Afya za Mijini”, ambao unalenga kusaidia serikali kupanga afya mijini kwa njia ya kimkakati na endelevu. Imesema ripoti hiyo ilitolewa  Geneva

“Huu ni wakati wa watunga maamuzi katika kila ngazi kushirikiana, mwongozo huu unawapa viongozi wa kitaifa na wa manispaa, wapangaji, wadau na jamii mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja katika sekta mbalimbali na ngazi tofauti ili kujenga mustakabali wa haki zaidi, wenye afya bora na uimara zaidi.” amesema Jeremy Farrar, Naibu Mkurugenzi mkuu wa WHO anayeshughulikia uendelezaji wa afya, kuzuia magonjwa na huduma za afya

Hatari na ukosefu wa usawa wa kiafya vinaonekana katika miji yote, utafiti wa miji 363 katika nchi tisa za Amerika ya Kusini ulionesha tofauti za matarajio ya maisha ya hadi miaka 14 kwa wanaume na miaka 8 kwa wanawake kati ya miji yenye afya bora na ile yenye afya duni. Wakazi wa miji wanakabiliwa na hatari nyingi zinazojirudia kuanzia uchafuzi wa hewa na usafiri usio salama hadi makazi duni, kelele na athari za hali ya hewa. Uchafuzi wa hewa pekee unasababisha vifo vya takribani watu milioni 7 kila mwaka, na karibu kila mkazi wa mji anavuta hewa isiyokidhi viwango vya ubora wa hewa vya WHO. Wingi wa watu unaongeza hatari ya milipuko ya magonjwa kama vile coronavirus“>COVID-19 na dengue, na upungufu wa maeneo ya kijani huongeza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Watunga sera wanashirikisha sauti za jamii moja kwa moja katika usanifu wa afya wa miji kama Dandora (Nairobi, Kenya), Suva (Fiji), Makassar (Indonesia), Coimbra (Ureno)  na miji mingine mingi.

“Miji ni nguzo kuu katika kuendeleza afya ya umma, mwongozo huu unawapa serikali ramani ya kimkakati ya kuchukua hatua, huku ukiunganisha moja kwa moja masuala mengine ya kimataifa kama mabadiliko ya tabianchi, usafiri, mabadiliko ya kidijitali na uhamiaji.” amesema Dkt. Etienne Krug, Mkurugenzi wa idara ya vihatarishi vya afya, kuzuia na uendelezaji wa afya katika WHO

Mwongozo huo unasisitiza kwamba afya si jukumu la sekta moja pekee, wala haitegemei tu maamuzi ya viongozi wa miji. Kuanzia hewa safi, makazi salama, usafiri unaochochea mwendo wa mwili, hadi upatikanaji wa huduma za kidijitali, pamoja na masuala ya fedha na udhibiti maamuzi yanayofanywa kila siku na mamlaka za miji katika sekta mbalimbali yanaathiri afya ya mabilioni ya watu. Kuchukua hatua za kimkakati  kunamaanisha kuunganisha maamuzi haya ili kujenga mustakabali wenye afya bora na usawa zaidi, ambapo mifumo ya mijini inafanya kazi pamoja kuimarisha usawa, uendelevu na uimara.

Kuchukua mtazamo wa kimkakati kwa afya za mijini  inaeleza hatua madhubuti kwa serikali ili:

·        Kuelewa ugumu wa mifumo ya mijini na jinsi inavyoathiri afya na usawa

·        Kubaini maeneo ya kuingilia kati, ikiwemo fursa za kujenga afya mijini kupitia sera na utekelezaji katika sekta nyingine

·        Kuimarisha njia za utekelezaji za afya mijini, zikiwemo utawala, ufadhili, takwimu, ubunifu, uimarishaji wa uwezo, ushirikiano na ushiriki wa jamii

·        Kuendeleza mikakati kamili ya afya mijini katika ngazi ya kitaifa na ya miji.

WHO inatoa wito kwa viongozi wa manispaa na wa kitaifa kutumia mtazamo wa kimkakati zaidi wa afya mijini, ikitambua nafasi muhimu ya serikali za mitaa na kitaifa katika kuunda hatua thabiti za kiafya zinazooana na malengo mengine ya kijamii, na kufanya miji kuwa si tu ya kuishi vizuri, bali pia yenye haki na endelevu.

Pamoja na mwongozo huu, WHO imezindua vipengele  vitatu za mwanzo za kozi ya kujifunza mtandaoni kuhusu afya mijini, kupitia  Chuo Cha WHO, ili kuimarisha uwezo wa kazi za pamoja katika mazingira ya mijini. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *