“Umoja wa Mataifa (UN), uko tayari kuunga mkono juhudi zinazolenga kuleta majadiliano, kuimarisha utawala wa kidemokrasia na kuendeleza amani endelevu nchini Tanzania,” aliongeza.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, pia iliripoti kuwa amri ya kutotoka nje nchini kote kuanzia saa kumi na mbili jioni inaendelea huku huduma za intaneti zikionekana kuwa na vikwazo vingi tangu siku ya kupiga kura.
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilizitaka mamlaka kurejesha huduma ya mtandao mara moja na kuwezesha wananchi kufikia kwa ukamilifu haki zao za msingi ikiwemo uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika kwa amani.
Waandamanaji pia walitakiwa kuandamana kwa amani.