
Ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Moscow na Beijing unaendelea licha ya vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya.
Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin atasafiri hadi Hangzhou Jumatatu ijayo kushiriki katika mkutano wa 30 wa wakuu wa serikali ya Russia na China.
Mkutano wa 30 wa kawaida kati ya wakuu wa nchi za Urusi na China utafanyika mjini Hangzhou siku ya Jumatatu. Baada ya mkutano huo, pande hizo mbili zitatia saini taarifa ya pamoja na hati kadhaa za pamoja. Mkutano wa 29 wa kawaida kati ya maafisa wakuu wa serikali hizo mbili ulifanyika huko Moscow mnamo Agosti 21, 2024.
Baraza la Mawaziri la Russia lilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa nchhi hiyo Mikhail Mishustin atakutana na Rais wa China Xi Jinping. Huduma ya vyombo vya habari ya serikali ya Russia imesema kuwa uhusiano wa kimkakati na ushirikiano kati ya Russia na China umefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa na unaendelea kuimarishwa kwa nguvu.