Kwanini China inalenga makanisa yasiyosajiliwaKwanini China inalenga makanisa yasiyosajiliwa

Hadi kufikia sasa ni makundi mawili tu ya Kikristo yanayotambuliwa rasmi nchini China:  Jumuiya ya Kikatoliki wa Wazalendo ya China pamoja na Vuguvugu la Wazalendo Watatu wa Kiprotestanti. Wakristo wanaoabudu nje ya mfumo wa makanisa yaliyoidhinishwa na serikali wanakabiliwa na kitisho hicho ambacho kinaonyesha kuongezeka kwa hali ya kutovumilia kwa uhuru wa kidini kwa Rais Xi Jinping.

Mapema mwezi huu, takriban wachungaji 30 na waumini wa Kanisa la Kiprotestanti la Sayuni, moja ya makanisa makubwa ya Kikristo yasiyo rasmi nchini China walikamatwa kufuatia msako ulioendeshwa kwenye takriban majimbo saba, akiwemo mwanzilishi wake, Jin “Ezra” Mingri.

Kwa mujibu wa mchungaji Bob Fu kutoka China ambaye alianzisha kundi la kidini lenye makao yake makuu huko nchini Marekani, amesema katika msako huo baadhi ya maafisa wa polisi walivamia makanisa hayo na kujifanya mafundi wa umeme na kufanya uharibifu kwenye kanisa huko China.

Israel | Marco Rubio
Rais wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio Picha: Fadel Senna/UPI Photo/IMAGO

Fu ameiambia DW kuwa ingawa kukamatwa kwa umati wa viongozi wa kanisa na wahudumu kumezua hofu miongoni mwa waumini wa Kanisa hilo, maisha wanayoyapitia ya uangalizi mkali yamewafanya wengi kuajiandaa kiakili kuikabili hali hiyo.

Mirro Ren, Mkristo wa Kichina anayeishi uhamishoni nchini Marekani, ameiambia DW kwamba hivi karibuni pamekuwepo na ongezeko kubwa la mashambulizi ya polisi dhidi ya makanisa yasiyosajiliwa nchini China kufuatia mfululizo wa kukamatwa na kufungwa kwa wachungaji ambao makanisa yao hayana ushirika na makanisa yanayotambulika na serikali ya Beijing.

China imeitaka Marekani kuacha kuingilia masuala yake ya ndani

Katika tarifa yake Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, ameikosoa hatua ya China kuwakamata viongozi wa makanisa na waamini wake akitaka kuachiliwa mara moja kwa wale wanaozuiliwa na kuwaruhusu watu wote wa imani zote kushiriki katika shughuli za kidini bila hofu ya kuadhibiwa.

Kwa upande wake, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lin Jian alinukuliwa na shirika la habari la Ujerumani la DPA akiitaka Marekani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Beijing.

Kwa muongo mmoja uliopita, Rais wa China Xi Jinping amesisitiza juu ya kuimarisha udhibiti wa kiitikadi juu ya makundi ya kidini na kuamuru kuvunjwa kwa makanisa na misalaba nchini humo kwa makanisa yasiyo na uhusiano na yale yanayotambuliwa na serikali.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za China iliyotajwa na Kituo cha Utafiti cha Pew, ni asilimia 2 tu ya idadi ya watu wa China kati ya watu milioni 29-44 ndio Wakristo. Lakini huenda takwimu hizo hazijumuishi washiriki wa makanisa yasiyofuata mfumo rasmi wa kuabudu ulioidhinishwa na serikali.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Global Christian Relief, kanisa la China ndilo linalokumbana na ukandamizaji zaidi ulimwenguni, huku uhuru wa kidini ukizorota chini ya utawala wa Rais Xi, tangu alipochukua madaraka mwaka 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *