Chini ya mwezi mmoja baada ya kupokea Tunzo ya Amani ya Nobel ya mwaka huu, kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado ambaye ni kibaraka wa Magharibi na muungaji mkono mkubwa wa jinai za Israel, sasa amewataka Wamarekani waishambulie kijeshi nchi yake.

Hayo yameripotiwa na Shirika la Habari la Fars ambalo pia limesema kuwa; Machado, ambaye ni mtu wa karibu sana na Benjamin Netanyahu na Donald Trump, amewataka Wazayuni wawashambulie kijeshi raia wa Venezuela akidai kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kumuondoa madarakani Rais Nicolas Maduro.

Aidha ameuambia mtandao wa habari wa Bloomberg wa Marekani kwamba: “Kuishinikiza zaidi Venezuela na kutumia nguvu za kijeshi dhidi yake ndiyo njia pekee ya kumlazimisha Maduro kuelewa kwamba anapaswa kujiuzulu.”

Matamshi hayo ya kichochezi ya kibaraka huyo wa Wazayuni yametolewa wakati huu ambapo mashambulizi ya kijeshi ya Marekani karibu na pwani ya Venezuela yameongezeka huku vyombo vya habari vikiripoti kuweko uwezekano wa kushambuliwa kijeshi raia wa Venezuela.

Gazeti la Miami Herald liliripoti jana usiku kwamba, Marekani inaweza kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya vituo muhimu vya Venezuela katika kipindi cha saa au siku chache zijazo.

Mwito wa Machado wa kushambuliwa Venezuela ni mwendelezo wa vitendo vyake vya kuifuata kibubusa Marekani bila ya kujali usalama wa raia wa nchi yake anaodai anawatetea.

Aidha katika kile kilichoonesha ni kutokuwa na thamani Tuzo ya Amani ya Nobel ambayo mwaka huu amepewa Machado, duru za habari zinasema kuwa, mara baada ya kupewa tunzo hiyo, Machado aliwapigia simu na Donald Trump na Benjamin Netanyahu na akamueleza Trump kwamba yuko tayari kumpa yeye tunzo hiyo ya Nobel.

Katika hatua nyingine ya kujipendekeza kupindukia na kutojali usalama wa raia wa Venezuela, Maria Corina Machado ametuma ujumbe kwa njia isiyo ya moja kwa moja na kuiambia Marekani kwamba ikiwa itamsaidia kumwondoa Maduro madarakani, yuko tayari kuhakikisha rasilimali nyingi za asili za Venezuela zinachukuliwa na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *