Kasri ya Mfalme wa Uingereza, Buckingham Palace, ilitangaza jana Ijumaa kwamba Andrew, kaka wa mfalme wa Uingereza, atajulikana kama Andrew Mountbatten Windsor na si Mwanamfalme, na hatakuwa tena na haki ya kutumia vyeo vyake vyovyote vya kifalme.

Kasri ya Buckingham imetangaza kwamba Mwanamfalme Andrew atapoteza vyeo vyake vya kifalme na kuondoka katika makazi yake ya Royal Lodge huko Windsor.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Mfalme Charles ameanza “mchakato rasmi wa kufuta vyeo na heshima zote za Prince Andrew” na sasa atajulikana kama Andrew Mountbatten Windsor.

Uamuzi huo umechukuliwa huku familia ya kifalme ya Uingereza ikiwa na wasiwasi kuhusu kuchafuliwa sifa ya familia hiyo, wakati huu ambapo vichwa vya habari kuhusu urafiki wa Mwanamfalme Andrew na mnyanyasaji wa watoto aliyekuwa mahabusu, Jeffrey Epstein, na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Virginia Giuffre, mmoja wa waathiriwa wa Epstein, yakiibua wasiwasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *