
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameitaja ziara yake ya hivi karibuni nchini Oman kuwa yenye manufaa.
Majid Takht-Ravanchi amesema jana Ijumaa kwamba: “Tunathamini sana mashauriano ya mara kwa mara na ndugu zetu wa Oman, na Muscat ni jirani wa kuaminika na mshirika muhimu wa Iran.”
Majid Takht-Ravanchi aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kuhusu safari yake ya Oman siku ya Alhamisi: “Baada ya safari fupi lakini yenye mafanikio Oman, nilirudi Tehran.” Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisiasa ameongeza kuwa: “Ilikuwa siku yenye shughuli nyingi mjini Muscat na nilikuwa na mikutano yenye manufaa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr al-Busaid na naibu wake Khalifa al-Harithi kuhusu masuala ya pande mbili, kieneo na kimataifa.”
Takht-Ravanchi, sambamba na kuashiria kwamba tunathamini sana mashauriano ya mara kwa mara na ndugu zetu huko Oman, alisema: “Pia nimekuwa na mikutano yenye manufaa juu ya Yemen na Mohammad Abdul Salam wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen na Hans Grundberg wa Umoja wa Mataifa.”
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehhusika na Masuala ya Kisiasa pia ameashiria kuwa, mkutano na waandishi wa habari na vyombo vya habari vya Oman na mkutano wa kirafiki na jamii ya Wairani wanaoishi Oman pia ilikuwa sehemu ya ratiba yake katika safari hiyo na akamalizia kwa kusisitiza: “Oman ni jirani wa kuaminika na mshirika wa kimsingi ambaye tuna uhusiano mzuri sana na uhusiano wa kihistoria.”