Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa urais uliofanyika wiki hii kulingana na matokeo rasimi ya leo Jumamosi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa Tanzania ulifanyika wakati wapinzani wakuu wa Rais Samia wakiwa wamefungwa jela wengine wakiwa wamezuiliwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Maandamano yamekuwa yakifanyika kwenye taifa hilo la Afrika mashariki tangu siku ya uchaguzi Jumatano ya wiki hii, mamia ya watu wakiripotiwa kufariki kwenye vurugu hizo za uchaguzi.

Kulingana na matokeo ya mwisho, Rais Samia ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 97.66 ya kura zote zilizopigwa, akitawala katika kila wilaya kama ilivyotangazwa na Tume ya uchaguzi kupitia runinga inayomilikiwa na serikali.

Vurugu za uchaguzi jijini Arusha nchini Tanzania Tanzanie, Tarehe 29 Oktoba 2025.
Vurugu za uchaguzi jijini Arusha nchini Tanzania Tanzanie, Tarehe 29 Oktoba 2025. AP

Kwa mujibu wa Televisheni inayomilikwa na serikali ya Tanzania, Rais Samia anaweza kuapishwa siku ya Jumamosi.

Chama kikuu cha upinzani, Chadema, kinasema maofisa wa usalama wamewaua mamia ya watu  tangu kuzuka kwa maandamano siku ya Jumatano ambayo ndio ilikuwa ni siku ya uchaguzi.

Hassan alichukua nafasi ya urais baada ya kifo cha mtangulizi, John Magufuli, mwaka wa 2021.

Chadema kilizuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ambapo kiongozi wake Tundu Lissu anagali anashikiliwa na polisi kwa mashtaka ya uhaini.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani chadema Tundu anazuiliwa kwa mashtaka ya uhaini
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani chadema Tundu anazuiliwa kwa mashtaka ya uhaini © Emmanuel Herman / REUTERS

Licha ya kuwepo kwa usalama mkubwa, siku ya uchaguzi iligubikwa na vurugu wakati waandamanaji walipoingia barabarani katika maeneo mbalimbali ya nchi, wakiharibu mabango ya Rais Samia, kukabiliana na polisi pamoja na kuvamia vituo vya kupiga kura.

Maandamano hayo yalipekea kukatwa kwa itaneti pamoja na kutangazwa kwa makataa ya watu kutembea nje.

Msemaji wa  Chadema wiki hii aliiambia AFP kuwa karibia watu 700 wameuawa kote nchini kwa mujibu wa takwimu walizopata kutoka kwa hosipitali tofauti na vituo vya afya.

Vurugu za uchaguzi katika eneo la Namnga upande wa Tanzania
Vurugu za uchaguzi katika eneo la Namnga upande wa Tanzania REUTERS – Thomas Mukoya

Chanzo cha kiusalama na kidiplomasia jijini Dar es Salaam nacho kimeiambia AFP kwamba mamia ya watu walikuwa wameuawa kwenye vurugu za uchaguzi.

Rais Hassan hajatoa taarifa yoyote kwa umma tangu kuzuka kwa vurugu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *