
Serikali ya Kongo imelaani siku ya Jumamosi, Novemba 1, upinzani wa kundi la M23 dhidi ya tangazo la rais wa Ufaransa la kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege wa Goma, mashariki mwa DRC, ambao uko chini ya udhibiti wa waasi wa M23 tangu wezi Januari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Alhamisi, Oktoba 30, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza wakati wa mkutano wa kimataifa mjini Paris uliojitolea kwa mgogoro katika eneo hilo, kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege wa Goma ili kurahisisha utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Tangazo hili, lililokaribishwa na Kinshasa, lilionekana kuwa “lisilofaa” na kundi la M23, ambalo lilisisitiza kwamba uamuzi wowote unapaswa kufanywa ndani ya mfumo wa mazungumzo yanayoendelea huko Doha, yanayosimamiwa na Qatar.