Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa mashambulizi ya Marekani katika eneo la Caribbean yanakiuka sheria za kimataifa.

Katika wiki za hivi karibuni Marekani ilizishambulia meli na boti ambazo ilidai zilikuwa zimebeba madawa ya kulevya na kuwa boti hizo zilitoka Venezuela.

Volker Turk alisema Ijumaa iliyopita kwamba: “Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, zaidi ya watu 60 wameuawa katika mashambulizi mtawalia ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya boti katika bahari ya Caribbean na Pacific kuanzia mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu. Mashambulizi haya hayawezi kuhalalishwa kivyovyote kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Mashambulizi haya na ongezeko la vifo vinavyotokana nayo, hayakubaliki. Marekani inalazimika kukomesha mashambulizi haya na kuchukua hatua zote muhimu ili kuzuia mauaji ya watu walio ndani ya boti hizo, bila kujali mwenendo wa uhalifu unaohusishwa nao.” 

Kama alivyoeleza afisa huyu wa Umoja wa Mataifa, sheria za haki za binadamu za kimataifa zinaeleza kuwa kutumiwa nguvu kubwa kunaruhusiwa tu kama suluhisho la mwisho na dhidi ya watu ambao wanatishia maisha ya wengine. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Marekani wamekiri kuwa hakuna abiria yoyote katika boti zilizoshambuliwa aliyekuwa tishio kwa maisha au aliyechukua hatua yoyote ambayo ingehalalisha matumizi ya nguvu kubwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Maduro ameokoka majaribio kadhaa ya kutaka kumuua yaliyofadhiliwa na Marekani.

Marekani imeendelea kuchochea mvutano kati yake na Venezuela kufuatia hatua yake ya kutuma askari wa jeshi la majini na anga katika eneo la Caribbean. Miezi miwili iliyopita, Wizara ya Vita ya Marekani (Pentagon) ilituma meli za kijshi, ndege za kivita, askari wa jeshi la majini, ndege zisizo na rubani (droni) na ndege za ujasusi katika eneo la Caribbean. Ndege za kivita aina ya B-52 pia zimefanya maneva ya hujuma karibu na pwani ya Venezuela. Aidha kwa kuzingatia kuongezeka mvutano kati ya Washington na Caracas, Trump ameidhinisha shughuli za siri za shirika la ujasusi la Marekani, CIA nchini Venezuela. Wiki iliyopita, Pentagon ilitangaza kuwa meli kubwa ya kubeba ndege za kivita ya USS Gerald R. Ford imeelekea katika eneo la Caribbean ikiambatana na kikosi chake cha oparesheni za anga..

Katika wiki za karibuni, mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani yalizamisha meli ambazo White House ilidai kuwa zilikuwa zimebeba mihadarati kutoka Venezuela.

Alipoulizwa kwamba je mashambulizi hayo yanaweza kuilenga ardhi kuu ya Venezuela katika siku zijazo au la, Trump alijibu kwa kusema: “Sitaki kuwaambia hasa kuhusu suala hilo.”

Kama alivyobainisha Rais Nicolas Maduro wa Venezuela, Trump ameanzisha makabiliano na nchi hiyo ya Amerika ya Kusini katika kalibu ya tishio kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika karne na hivi karibuni na ametangaza uwezekano wa kufanyika mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya Venezuela. Marekani inamuhusisha Nicolas Maduro na genge la wauzaji wa dawa za kulevya linalojulikana kwa jina la “De los Soles” (The Cartel of the Suns) na kuongeza dau la kitita cha pesa kama zawadi kwa mtu yeyete yoyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kutiwa kwake mbaroni kutoka dola milioni 25 hadi milioni 50 kwa.

Pamoja na hayo, Rais wa Marekani Donald Trump Ijumaa wiki hii alikanusha ripoti za mpango wa kuishambulia Venezuela na kusema: Hata hivyo Rais Nicolas Maduro wa Venezuela anaamini kinyume chake hasa kwa kuzingatia rekodi mbaya ya upotoshaji na kukiuka ahadi kwa Trump. Maduro amesema: Kukanusha Trump kuhusu mpango wa shambulizi dhidi ya Venezuela mara hii kumezidisha imani miongoni mwa wananchi kwamba Washington inapanga njama dhidi ya nchi yao. “Kila kitu kinachofanywa dhidi ya Venezuela kinafanyika kwa lengo la kuhalalisha vita, kubadili serikali na kupora utajiri wetu wa mafuta”, amesema Rais wa Venezuela.

Marco Rubio Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani pia siku ya Ijumaa alizungumzia ripoti iliyodai kuwa serikali ya Trump imeamua kuzishambulia taasisi za kijeshi za Venezuela. Rubio aliandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: “Vyanzo vya ripoti hiyo vinavyodai kuwa vina taarifa kuhusu hali ya mambo ni vya vimewadanga na kutoa taarifa za uwongo”. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameeleza haya akijibu ripoti ya gazeti la Miami Herald iliyosema kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Venezuela yanaweza kuanza “wakati wowote” na kwamba Washington imedhihirisha msimamo wa kichokozi zaidi dhidi ya Venezuela.

Rais Nicolas Maduro anaituhumu serikali ya Marekani kuwa ina mpango wa kupindua serikali yake.

Mbali na Miami Herald, jarida la Wall Street liliripoti siku ya Alhamisi kwamba utawala wa Trump umetambua vituo vya kijeshi nchini Venezuela vinavyotumika kwa ulanguzi wa dawa za kulevya kama maeneo ambayo huwenda yakashambuliwa. Chombo hicho cha habari kiliongeza kuwa Trump bado hajafanya uamuzi wa mwisho wa kutekeleza mashambulizi hayo.

Licha ya kukanushwa na maafisa wa Marekani, inaonekana kwamba Trump ameazimia kushambulia Venezuela kwa kisingizio cha kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya kwenda Marekani. Utangulizi wa hatua hiyo ni mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya meli na boti ambazo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hazikuwa tishio lolote kwa maisha ya binadamu waka hazikuchukua hatua yoyote ambayo ingehalalisha matumizi ya nguvu hatari chini ya sheria za kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *