Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amemkosoa vikali Donald Trump, akiutaja utawala wake kuwa ni “kielelezo cha uasi na mparaganyiko” na kuwashutumu Warepublican kwa kukaa kimya mbele ya mienendo yake ya kutowajibika.

Akizungumza katika mikutano ya kampeni huko Virginia na New Jersey, Barack Obama amewahimiza watu kusimama kidete dhidi ya sera za Trump kwa kuwapigia kura Wademokrasia.

Amesisitiza umuhimu wa uchaguzi ujao nchini Marekani na kusema, “Marekani iko katika kipindi cha giza na kila siku tunashuhudia wimbi jipya la ukatili na uvunjaji sheria kutoka Ikulu ya White House.”

Obama ameitaja sera za ushuru za Trump kuwa “zilizovurugika” na kwamba kupelekwa Gadi ya Taifa katika miji ya Marekani ni “ishara ya hofu na kutokuwa na mantiki.” Ameongeza kuwa: “Warepublican hubaki kimya hata wanapojua kwamba Trump amevuka mstari mwekundu; baadhi ya makampuni na taasisi pia zimepiga magoti mbele yake kwa ajili ya kulinda maslahi yao.”

Obama ametoa matamshi ya kejeli kuhusu gharama za masuala ya anasa na ya kifahari za Ikulu ya White House katika utawala wa Trump na kusema: “Trump anajishughulisha zaidi na miradi muhimu, kama vile kuweka lami kwenye Bustani ya Waridi (Rose Garden) na kujenga ukumbi wa kunengua wa dola milioni 300!”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *