Picha mpya za setilaiti na ushuhuda kutoka kwa shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) zinaonyesha Jumamosi, Novemba 1, kwamba mauaji yanaendelea katika jiji la Sudan la El-Fasher, magharibi mwa Sudan, karibu wiki moja baada ya kuwa chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati ripoti za vurugu dhidi ya raia zikiongezeka, mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani na Uingereza wameonya kuhusu hali ya “uharibifu mkubwa” na “ya kutisha kabisa” katika mji wa El-Fasher ulio chini ya udhibiti wa RSF.

Baada ya kuzingirwa kwa miezi 18, wanajeshi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, anayejulikana pia kama Hemedti, waliteka mji wa El-Fasher siku ya Jumapili, Oktoba 26. El-Fasher ulikuwa mji mkuu wa mwisho huko Darfur (magharibi mwa Sudan) ambao ulikuwa uliepuka kuwa chini ya udhibiti wao katika vita vyao dhidi ya jeshi la Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan.

Kulingana na Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Yale (ripoti inapatikana hapa), ambayo inachambua video na picha za setilaiti, picha za hivi karibuni kuanzia siku ya Ijumaa hazionyeshi shughuli nyingi za raia huko El-Fasher, ikimaanisha kwamba idadi kubwa ya wakaazi wake wamefariki, wamekamatwa, au wamejificha.

Maabara hiyo ilitambua angalau makundi 31 ya vitu vinavyofanana na miili ya binadamu kati ya Jumatatu na Ijumaa katika vitongoji mbalimbali, kwenye vyuo vikuu, na katika maeneo ya kijeshi. “Ishara zinonyesha kwamba mauaji yanaendelea bila shaka,” imehitimisha.

Idadi kubwa ya watu walio katika “hatari kubwa ya kifo,” kulingana na MSF

Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) pia wamesema siku ya Jumamosi kwamba wana hofu kuwa “idadi kubwa ya watu” bado wako “katika hatari kubwa ya kifo” na kwamba raia walikuwa wakizuiwa na RSF na washirika wao “kufikia maeneo salama” kama vile Tawila. Maelfu ya watu tayari wamekimbia El-Fasher kwa mji huu ulioko yapata kilomita 70 upande wa magharibi, ambapo MSF imejiandaa kukabiliana na wimbi kubwa la watu waliokimbia makazi yao na waliojeruhiwa.

Walionusurika wameiambia MSF kwamba wakazi walitenganishwa kulingana na jinsia zao, umri, au utambulisho wa kikabila unaodhaniwa, na kwamba wengi bado wanashikiliwa kwa ajili ya fidia. Mmoja wa manusura ameripoti “matukio ya kutisha” ya wafungwa wakikanyagwa na magari ya wapiganaji.

“Idadi ya watu waliofika Tawila ni ndogo sana… Wako wapi watu wote wanaokosekana ambao wamenusurika miezi kadhaa ya njaa na vurugu huko El-Fasher?” ana wasiwasi Michel-Olivier Lacharité, mkuu wa shughuli za dharura katika sirka la MSF.

“Tuna hofu ya kutokea hali mabaya zaidi…”

“Madaktari Wasio na Mipaka, tuliondoa timu zetu kutoka El-Fasher mnamo mwezi Aprili 2025. Na kwa hivyo sasa, tuna wafanyakazi wapatao 500 wanaofanya kazi katika hospitali katika mji wa Tawila, kilomita 60 kutoka El-Fasher. Tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, timu hizi zimekuwa zikipokea watu waliochoka, wenye njaa, na waliojeruhiwa waliofika kutoka El-Fasher.” Ingawa mwanzoni mwa wiki kulikuwa na idadi kubwa ya majeruhi na makumi ya maelfu ya watu waliofika, wimbi wa watu wanaowasili limepungua haraka sana. Hii inatufanya tuamini, na hii pia ni ushuhuda wa wale waliowasili, kwamba idadi kubwa ya watu wanashikiliwa njiani, na tuna hofu ya kutokea hali mabaya zaidi. Hatujui kama wameuawa au kama kumekuwa na umwagaji damu. Maelfu ya watu hawajulikani, na ni kwa maana hii kwamba taarifa yetu inaonyesha wasiwasi kwa makumi ya maelfu ya watu ambao hawajulikani walipo,” Michel-Olivier Lacharité ameambia RFI.

Doctors Without Borders, tumeanzisha kituo cha matibabu cha hali ya juu ili kutoa chakula, maji, na vifaa vya lishe kwa wale wanaowasili. Ikumbukwe kwamba tumeona watu wazima ambao walikuwa na utapiamlo. Tumeona kwamba takriban 40 hadi 50% ya watoto wanaowasili kutoka El-Fasher wana utapiamlo, kwani jiji hilo lilizingirwa kwa zaidi ya siku 500. Pia tumewatibu wengi waliojeruhiwa. Katika siku chache za kwanza, tulipokea waathiriwa zaidi ya mia moja wa risasi kwa siku. Pia tuna waathiriwa wa mateso. Simulizi tunazopata kutoka kwa watu wanaowasili kutoka El-Fasher zinaelezea vurugu zenye misingi ya kikabila. Baadhi ya makundi ya watu yanatengwa, na wengi wanapigwa. Tumesikia ripoti za mateso. Baadhi ya watu wanasema wamenyofolewa macho, na pia kumekuwa na mauaji ya halaiki. Hii inatuweka katika hali ya wasiwasi mkubwa kuhusu hatima ya watu katika mji wa El-Fasher.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *