Umoja wa Afrika umepongeza rais anayemaliza mda wake nchini Tanzania, Samia Suluhu Hassanambaye alishaguliwa tena hivi karibu kwa muhula mwigine kwa ushindi wake.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika, AU umepongeza ushindi wa Samia Suluhu Hassan, na kusikitishwa na vurugu zilizokumba maeneo kadhaa nchini Tanzania. Upinzani unadai kwamba watu karibu 800 waliuawa katika machafuko hayo.

Vurugu za uchaguzi jijini Arusha nchini Tanzania Tanzanie, Tarehe 29 Oktoba 2025.
Vurugu za uchaguzi jijini Arusha nchini Tanzania Tanzanie, Tarehe 29 Oktoba 2025. AP

Vurugu zilizoikumba Tanzania kwa muda wa siku tatu baada ya uchaguzi huo, hazikuzuia Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, INEC, kumtangaza Samia Suluhu Hassan mshindi wa uchaguzi huo. Samia Suluhu Hassan ameibuka mshindi wa uchaguzi wa urais kwa 98 ya kura. 

Baada ya kupokea cheti cha ushindi wa urais kutoka kwa mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi Tanzania INEC, Jacobs Mwambegele, jana Jumamosi, Rais Samia Suluhu Hassan aliyakosoa maandamano yaliyopinga zoezi la uchaguzi na ambayo yaliitikisa Tanzania kwa siku tatu mfululizo.

“Tunavishukuru vikosi vya usalama kwa kuhakikisha kuwa vurugu hazikuzuwia upigaji kura. Serikali ikalaani machafuko yaliyotokea,” alisema rais Samia akiongeza kuwa matukio hayakuwa yakizalendo hata kidogo.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yamesema yalishuhudia wivi la vurugu za kutisha  katika taifa hilo la Afrika Mashariki kabla ya uchaguzi huo kufanyika ikiwemo kutekwa kwa wanasiasa wa ngazi ya juu kulikokithiri katika dakika za mwisho kabla ya zoezi hilo la Oktoba 29.

Gari la polisi ya Tanzania likiendeshwa kando ya barabara iliyozuiliwa na waandamanaji wakati wa maandamano yaliyokumbwa na vurugu jijini Dar es Salaam, Tanzania, mnamo Oktoba 29, 2025.
Gari la polisi ya Tanzania likiendeshwa kando ya barabara iliyozuiliwa na waandamanaji wakati wa maandamano yaliyokumbwa na vurugu jijini Dar es Salaam, Tanzania, mnamo Oktoba 29, 2025. © Onsase Ochando / Reuters

Hata hivyo vyanzo vya usalama vinabaini kwamba hali ya utulivu imerejea nchini kote tangu jaa Jumamosi.

Maandamano hayo yalipekea kukatwa kwa intaneti pamoja na kutangazwa kwa makataa ya watu kutembea nje

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *