
Serikali ya Lecornu haitaingia katika mvutano na Algeria, ambayo bado inawashikilia raia wawili wa Ufaransa katika magereza yake (mwandishi Boualem Sansal na mwandishi wa habari Christophe Gleize) na inakataa kuwachukua raia wake waliofukuzwa. Ingawa chama cha RN kilipitisha muswada wiki hii katika Bunge la taifa unaotaka kumalizika kwa makubaliano ya mwaka 1968, Waziri wa Mambo ya Ndani Laurent Nuñez anaomba katika Gazeti la Le Parisien “ushirikiano mzuri na wenye tija” na Algiers.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Je, anaogopa kwamba hali itakuwa mbaya zaidi baada ya kura ya wiki hii katika Bunge? Kwa vyovyote vile, Waziri wa Mambo ya Ndani Laurent Nuñez anajitofautisha waziwazi na mtangulizi wake, Bruno Retailleau, kiongozi wa chama cha Republican cha mrengo wa kulia (LR), anayejulikana kwa matamshi yake makali. Bila kumtaja moja kwa moja, ameliambia Gazeti la Le Parisien: “Wale wanaowafanya Wafaransa waamini kwamba makabiliano na mbinu za kikatili ndio suluhisho pekee wanatuweka hatarini.”
Ametaja, haswa, uhusiano wa kiusalama na Algiers, ambapo Paris haiwezi kutekeleza yenyewe, lakini pia, amesema, ukosefu wa matokeo. “Mvutano hauna nafasi.” Kama “uthibitisho” wa kutofanikiwa kwa njia hii, ameongeza, “uhusiano sio mzuri kabisa leo na Algiers.”
Laurent Nuñez anapendelea mazungumzo
Laurent Nuñez pia ameelezea masikitiko yake kuona Algeria haiwarudishi tena raia wake waliofukuzwa nchini Ufaransa. Mnamo mwaka 2025, uhamisho wa kulazimishwa wa watu 500 kutoka Ufaransa kwenda Algeria ulifanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba, ikilinganishwa na watu 1,400 wakati wa kipindi kama hicho mwaka jana, kulingana na waziri. Kwa hivyo, vituo vya Ufaransa wanakozuiliwa wahamiaji “viko vimejaa kabisa”: “Asilimia 40 ya watu hao ni kutoka Algeria.”
Akiwa amekaa ofisini kwa siku 20 tu, ni wazi bado hawezi kuwasilisha matokeo halisi, lakini anahakikisha kwamba nia yake iliyotajwa alipofika wizarani, akipendelea mazungumzo, inapiga hatua. Anafichua kwamba hivi karibuni alialikwa na mwenzake wa Algeria, Saïd Sayoud.
Mikataba ya 1968 iliyoshutumiwa katika Bunge la taifa
Lakini mshtuko uliosababishwa na kupitishwa Alhamisi, Oktoba 30, kwa azimio la kushtumu mikataba ya mwaa 1968 kati ya nchi hizo mbili unatatiza kuanza kwa mazungumzo.
Mkataba huo, uliosainiwa miaka sita baada ya kumalizika kwa vita na koloni lake la zamani, uliunda mfumo mzuri wa uhamiaji kwa Waalgeria, ambao hawahitaji visa maalum ili kukaa zaidi ya miezi mitatu nchini Ufaransa na wana ufikiaji wa haraka zaidi kuliko wageni wengine wa vibali vya ukaazi vya miaka 10, ikiwa ni pamoja na kupitia kuungana tena kwa familia. Kauli yake inadaiwa kwa muda mrefu na vyama vya mrengo wa kulia nchini Ufaransa.