
Uturuki itaendelea kuimarisha miradi yake ya kiulinzi na maslahi na washirika wake wa Ulaya, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema.
“Wakati tukiweka kipaumbele kwenye miradi yetu ya kiulinzi, tutaendelea kuongeza ushirikiano na washirika wetu wa Ulaya kwa maslahi ya pande zote,” alisema Erdogan wakati wa mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu mara baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri jijini Ankara.
Akianisha baadhi ya miradi hiyo kama vile ule wa ndege za kivita maarufu kama KAAN, Erdogan aliweka wazi kuwa ndege hizo zitakuwa sehemu ya “Jeshi la Anga la Uturuki”.