Israel siku ya Jumapili imepokea miili ya mateka wengine watatu waliofariki ambao Hamas imesema ni mateka wengine watatu waliofariki huko Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Miili hiyo imekabidhiwa Israel kupitia shirika la Msalaba Mwekundu na kupelekwa katika maabara ya kitaifa ya uchunguzi wa kimatibabu nchini humo kwa ajili ya utambuzi.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema mwili wa raia wa Israel mweny asili ya Marekani, Omer Neutra, ulikuwa miongoni mwa mateka waliofariki ambao Hamas iliikabidhi Israel siku ya Jumapili.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege ya rais ya Air Force One akiwa njiani kuelekea Washington, Trump amesema alizungumza na wazazi wa Neutra. “Wamefurahi, kwa maana moja, lakini kwa maana nyingine, ni wazi, si jambo kubwa sana, lakini tunafurahi sana kufanya hivyo,” amesema.

Uhamisho wa hivi karibuni wa mabaki unakuja baada ya Hamas kukabidhi miili ya mateka wawili waliofariki siku ya Alhamisi jioni, waliotambuliwa kama Amiram Cooper, 84, na Sahar Baruch, 25.

Hamas pia ilikabidhi mwishoni mwa jumaa miili ya watu watatu waliofariki, lakini haikutambuliwa kama ya mateka yeyote aliyefariki, afisa wa Israel alisema siku ya Jumamosi.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Jumapili kwamba Israeli imejitolea kuhakikisha mateka wote waliofariki wanarudi. Akizungumza katika mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri, Netanyahu aliishutumu Hamas kwa “majaribio ya kusikitisha ya kutudanganya sisi, Marekani, na dunia. Bila shaka, itashindwa, na hatua kwa hatua tutawarudisha mateka wetu wote.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *