Musa Idris, mkulima kutoka Jimbo la Jigawa, lililoko kaskazini mwa Nigeria, maarufu kwa kilimo, hasa cha mpunga, ngano, mtama na mboga mboga, anasema Kabla ya mradi huu, tulikumbwa na changamoto ya uhaba wa maji.

Akiwa shambani mwake akiliandaa kwa ajili ya upanzi Musa anaelezea mabadiliko baada ya Benki ya Dunia kuingilia kati.

Sasa tunapata maji zaidi. Tunatayarisha shamba kupanda nyanya na mpunga, na baada ya hapo tutaandaa shamba kwa ajili ya ngano. Awali tulivuna magunia 15 hadi 20 ya mpunga kwa ekari, sasa tunapata magunia 30 hadi 35.”

Je Benki ya Dunia ilifanya nini? Ni kwamba kupitia mradi wa Kuboresha na Kusimamia Shughuli za Umwagiliaji nchini Nigeria (TRIMING), unaotekelezwa na Benki ya Dunia kwa ushirikiano na Wizara ya Rasilimali za Maji na Usafi wa Mazingira nchini humo, mradi umeboresha mifumo ya umwagiliaji, ukiongeza eneo la umwagiliaji hadi zaidi ya ekari 37,000 — na kunufaisha zaidi ya watu milioni moja.

Ramatu Isah Umar, Naibu Kiongozi wa kikundi cha wanawake jimboni Kano nchini Nigeria. Yeye ni mkulima na mnufaika wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji.

© World Bank

Ramatu Isah Umar, Naibu Kiongozi wa kikundi cha wanawake jimboni Kano nchini Nigeria. Yeye ni mkulima na mnufaika wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji.

Mradi pia umewezesha wanawake kupata maji ya matumizi ya kila siku. Miongoni mwao ni Ramatu Isah Umar, Naibu Kiongozi wa kikundi cha wanawake jimboni Kano, jirani na Jigawa.

Zamani, tulikuwa tukilima ekari 22 tu za mashamba lakini kwa sasa tunalima na kuvuna zaidi ya ekari 22. Na haya mafanikio yametuwezesha hadi kwa sasa watoto wetu wanakwenda shuleni. “

Kadri mahitaji ya chakula duniani yanavyoongezeka, Benki ya Dunia inaendelea kusaidia miradi kama TRIMING — ili kuwezesha wakulima katika kuzalisha mazao zaidi, na kujenga mustakabali salama wa chakula kwa Nigeria na dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *